wahusika katika kigogo na Umuhimu na sifa zao

10 min read

wahusika katika kigogo na sifa zao 
 MAJOKA

 • Ni kiongozi wa jimbo la Sagamoyo.
 • Ni mumewe Husda.
 • Ni babake Ngao Junior.
 • Ni mwanawe Bw.Marara.
 • Ni mjukuu wake Ngao.
 • Ni mmiliki wa Majoka and Majoka company,Majoka and Majoka resort na Majoka Academy.

Sifa zake

 • Ni katili-Anapanga jama ya kumlemaza Tunu.Pia anawaagiza askari kuwatawanya waandamaji wanaotetea sosko la Chapa kazi.
 • Pia anawatuma "chatu” kumwangamiza Ngurumo.
 • Ni fisadi-Anamtuma Bw.Kenga na "keki” kwa Sudi ,Boza na Kombe ,ndiposa wamchongee vinyango.
 • Ni mkware-Ingawa ana bibi Husda ,anamtamani sana Ashwa bibiye Sudi na kujaribu kumshawishi ampe uroda.
 • Ni mpyoro-Anapenda kutumia maneno ya matusi sana."shut up ! woman wasaliti nyinyi hamna shukrani hata mpigieni huyo Tunu wenu kura tuone hata msiponipa kura moja nitashinda.” (uk.91).
 • “Utakaa hapa name ,sitaki hawa makunguru wanidhuru.”( uk 38)
 • Ni Jasiri-Anaujasiri wa kujitokeza kaika umati wa watu hata kama amewakosea na wamekasirika naye.
 • Ni mwizi-Anatumia cheo chake kunyakua mali ya umma.Anafunga soko la chapakazi kwa lengo la kujenga hoteli la kifahari.
 • Ni mbinafsi-Anatia maslahi yake mbele ya matakwa ya wanasagamoyo waliomchagua.
 • Ni mwenye majuto-Baada ya kuzirai aliposikia kifo cha mwanawe Ngao Junior ,katika ule uigizaji wa kiepiki anajuta matendo ya nafsi yake na kumwomba babu yake ushauri.
 • Ni msiri-Anahifadhi siri nyingi ambazo hataki kuzielekeza moja kwa moja kama vile uhusiano wake na Ashua ,unyakuzi wa mali ya umma kuendeleza kampuni ya Majoka and Majoka company n.k

Umuhimu wake

 • Ni kielelezo cha viongozi wasiowajibika katika uongozi wao haswa barani Africa .Viongozi wanaotumia mamlaka yao kujitayarisha na kulidhi mahitaji yao ya kibinafsi.
 •  Ametumiwa kuukashifu mfumo wa ugatuzi unaoongozwa na viongozi wenye tama ya fisi.

 TUNU

 • Ni mwanamapinduzi
 • Ni mwanawe Hashima
 • Ni rafiki yake Sudi,Ashua na Siti.

Sifa zake

 • Ni mwenye utu-Anaongozwa na utu kuzipigania haki za kimsingi za wanaSagamoyo
 • Ni msomi-Amesoma na kuhitimu chuo kikuu kule Ng'ambo.Ili linatokea katika kejeli ya wimbo wake Daudi Kabaka aliouimba Ngurumo.
 • “Msichana mrembo kama wewe ni kitu gani kinachofanya usiolewe,elimu unayo ya kutosha hata Ng’ambo ulieda ukarudi.”(uk 65)
 • Ni jasiri-Anapambana na Majoka kwa ujasiri na kukashifu matendo yake hata baada ya kulemazwa na genge alilolituma Majoko lililoongozwa na Ngurumo.
 • Ni mwenye mapenzi ya dhati-Anawajali watoto wake Sudi (Pendo na Pili) na kumwagiza Siti awapeleke kwa mamake ili awatunze .(uk 18)
 • Ni mwana mapinduzi-Anashiriki katika harakati za kuikomboa Sagamoyo kutoka mikononi mwa Kigogo Majoka.
 • Ni mrembo-Urembo wake unajidhihirisha kutokana na kejeli yake Ngurumo kutoka kwa wimbo wake Daudi Kabaka.

Umuhimu wake

 • Ni kielelezo cha vijana waliosoma wanaoshiriki katika harakati za mapinduzi na kuzikomboa nchi zao kutoka mikonini mwa vigogo dhalimu.
 •  Ni kielelezo cha wananchi jasiri wanaojitolea kufa kupona kwa ajili ya haki z kibinadamu.
 •  Yey kulemazwa ni dhihirisho la watu ambao wako tayari kupatwa na lolote kwa minajili ya ukombozi wa nchi zao.


sifa za wahusika katika
wahusika na sifa zao
wahusika na sifa zao katika tamthilia kigogo
sifa za boza katika kigogo
umuhimu wa asiya katika kigogo
kigogo maudhui
sifa za babu katika kigogo
umuhimu wa kombe katika kigogo 

SUDI

 • Ni mchonga vinyago.
 • Ni mumewe Ashua.
 • Ni babake Penda na Pili
 • Ni rafikiye Tunu na Siti.

Sifa zake

 • Ni msomi-Amesoma na kuhitimu chuo kikuu.
 • Mwenye bidii-Anafanya kazi ya kuchonga vinyago ndiposa awezi kukimu mahitaji ya familia yake.
 • Ni mwenye mapenzi ya dhati-Anampenda bibiye Ashua kwa moyo na mapenzi ya dhati.
 • Anaenda kumtembelea anapofungwa na Majoka.
 • Ni jasiri-Anapigania haki za wanaSagamoyo bila woga wowote na kuwakabili Majoka na vikaragozi wake moja kwa moja ,kwa ushujaa mwingi .”Mimi sili makombwe kama kelbu ,nishakunywa chai ya mke wangu nikariridhika.”(uk 13)
 • Ni mwenye utu-Anajali maslahi ya wanasagomoyo waliofungiwa soko la chapakazi ndiposa anashiriki katika harakati za kutetea ufunguzi wa soko lile.
 • Ni mkweli-Anamsimamo dhabiti na anawatambua mashujaa halisi wa Sagamoyo .”Nawe muugwana wamchonga nani?” “Shujaa halisi wa Sagamoyo.” (uk 10)
 • Ni mwanamapinduzi-Anashiriki katika harakati za kumnyanyua kigogo Majoka.

Umuhimu wake.

 •  Ni kielelezo cha watu wenye bidii maishani wanaofanya kazi kukimu mahitaji ya familia zao.
 •  Pia ni kielelezo cha wasomi wanashiriki katika harakati za ukombozi wan chi zao kutoka mikononi mwa vigogo.

 ASHUA

 • Ni bibiye Sudi.
 • Ni mamake Pendo na Pili.
 • Ni rafikiye Siti na Tunu.

Sifa zake

 • Ni mwenye bidii-Anafanya kazi kwa bidii ndipo aweze kukidhi mahitaji ya familia yake.”Ndio hali ya maisha bibiye tena lazima tutie tonge kinywani na tuwape wananchi wenye nchi kitu kidogo .Biashahara iko vipi kwenye vioski vyenu?”(u.k 2)
 • Ni mlezi mwema-Anafanya kila juhudi ndipo aweze kuwalea wanawe Pendo na Pili tendo linalompeleka ofisini mwa Majoka.
 • Ni mwenye utu-Anamsimamo dhabiti na kukataa rai zote za Majoka ikiwemo ile ahadi ya kupewa kazi katika shule ya Majoka and Majoka Academy .”Siwezi ,siwez kufanya kazi kweny kampuni ya kihuni kama hiyo mimi.” (uk 25)
 • Ni msomi-Amesoma na kuhitimu chuo kikuu.”Na hiyo ndio shida hasa ! Takwimu zako wazitoa visivyo .Ulipofuzu nilikupa kazi katika Majoka Academy ukakataa.Shahada yako ya ualimu ukataka iozee huko sokoni .Sasa ungekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule zetu za kifahari.Maisha yako yangkuwa tofauti kabisa .Utayakaanga marimgo yawe kitoweo wewe siku moja ! (u.k 25)
 • Ni mwanamapinduzi-Anashirikiana na mumewe Sudi ,Tunu na Siti katika harakati za kuikomboa Sagamayo kutoka mikononi mwa kigogo Mojoka .Katika ule mkutano pale sokoni anaongoza katika wimbo wa mapinduzi(uk.92) “Soko lafunguliwa bila nyoka ×2 Soko lafunguliwa bila chopi ×2
 • Ni mrembo-Ana urembo ambao unamvutia sana bwana Majoka na kumtia hamu ya uroda.

Umuhimu wake

 • Ni kielelezo cha wanawake wanaopitia changamato kuu katika ndoa zao sababu ya kupingana na uongozi dhalimu.
 • Pia ni kilelezo cha wasomi wanaokosa kazi kwa sababu ya kushikilia msimamo dhabiti.

 SITI

 • Ni dadake Kombe.
 • Ni rafikiye Tunu ,Sudi na Ashua.

Sifa zake

 • Ni rafiki wa dhati-Anashirikiana na Tunu katika hali zake zote hata anapokuwa mlemavu Siti yuko pale kumsaidia
 • Ni mwanamapinduzi-Anashirikiana na Tunu ,Sudi na Ashua kumnyanyua kigogo Majoka.
 • Ni mwenye msimamo dhabiti-Anapoiacha pombe na angali nyuma hata baada ya kushawishiwa na Ngurumo kushiriki katika unywaji wa pombe .”Nawaelewa msitafune maneno sote tulianza kama nyinyi .Safari ni hatua kwa hatua (kwa Siti)Do ! Sitiiii……..nilijua utarudi ,umekumbuka zabibu….”sikuja kunywa pomb mie ,niliacha……(uk 57)

Umuhimu wake

 • Ni kielelezo cha marafiki wa dhati walio simama na watu katika hali zote kufa kupona.

 BOZA

 • Ni mumewe Asiya
 • Ni kikaragozi cha Majoka
 • Ni mchonga vinyago.

Sifa zake

 • Ni kikaragozi-Anamtumikia na kumpigia upato Bwana Majoka ambaye ni kiongozi dhalimu.
 • Ni mwenye bidii-Anafanya kazi ya kuchonga vinyago.
 • Ni mlevi-Anashiriki pombe inayopikwa na bibiye Asiy (Mama Pima)
 • Ni mkengeuzi-Anamruka kombe na kumnyima haki yake waliyopewa na Bw Kenga.``Salamu zako tulizipokea mzee na tuko katika……”maneno ya Boza.
 • “Salamu gani ?”Maneno ya Kombe.(uk 9)

Umuhimu wake

 •  Ni kiwakilishi cha watu wanaowatumikia na kuwanyenyekea viongozi bila kutazama ukweli uliopo.

 KOMBE

 • Ni kakake Siti.
 • Ni mchanga vinyago.

Sifa zake

 • Ni mwenye bidii-Anafanya kazi ya kuchonga vinyago
 • Ni kikaragozi-Anampigia madebe kigogo Majoka.
 • Ni mwenye kushawishika haraka-Anashawishika na Sudi na kubadili msimamo wake kumhusu Majoka.

Umuhimu wake .

 •  Ni kielezo cha watu wa kawaida katika jamii wanaopotozwa na uongozi mbaya lakini baadaye wanazidiwa baada ya kupata ukweli wa mambo.

 NGURUMO

 • Ni kikaragozi cha Majoka.

Sifa zake

 • Ni kikaragozi-Anamtumikia na kumpigia debe kigogo Majoka.
 • Ni mkware.-Anashirika urada na mama Pima ambaye ni bibiye Boza .”Wako au wa Ngurumo.” Maneno ya Sudi
 • “wetu sote pili pili usioila yakuashia ni?” (uk 64)
 • Ni mlevi-Anashiriki ulevi wa pombe kwa mama Pima na ndiye anayewaongoza walevi wengine.
 • Ni katili-Anawaongoza vijana wngine kumvamia Tunu kwa maagizo ya Bw Majoka .”Mimi nina shughuli zangu Tunu ,hayo aliyoyasema tulishayajua na hayajatushtua.Tafadhali nenda kama hutaki…….Hakuna asiyejua .(Akiashiria miguu ya Tunu)Nilifikiri hila ni funzo tosha.”maneno ya Ngurumo (uk 63)

Umuhimu wake

 •  Ni kiwakilishi cha vijana ambao wanatumiwa na viongozi kuendeleza uongozi dhalimu.
 •  Ni kilelezo cha vijana ambao hawashiriki katika shughuli za kujnga taifa hila wanashiriki ulevi.

 KENGA

 • Ni msichana mkuu wa Majoka.

Sifa zake

 • Ni kikaragozi-Anamtumikia kigogo Majoka bila kuwajali wanasagomoyo.
 • Ni katili-Anashiriki katika kupanga jama ya kumlemaza Tunu.
 •  Ni binafsi-Anayajali maslahi yake mwnyewe ndio maanake anamshauri Majoka bila kujali hisia za wahasagamoyo wa kawaida .Lengo lake kuu ni kushibisha tumbo lake na kupata sehemu kubwa ya “keki.”
 • Ni mshauri mbaya-Anampa Bw Majoka ushauri mbaya wa kupotosha.
 • Ni mkengeuzi-Mambo yanapoharibika anamgeuka Majoka na kuwaunga mkono wanasagamoyo wa kawaida.
 •  Ni mwenye busara-Ana busara nyingi ingawa anaitumia vibaya kumshawishi Sudi kumtumikia Majoka.

Umuhimu wake

 • Ni kielezi cha watu wanaotoa ushauri mbaya kwa viongozi na mambo yakienda mrama wanawageuka.

 MAMA PIMA (ASIYA)

 • Ni bibiye Boza.
 • Ni mgema .

Sifa zake

 •  Ni kikaragozi-Anamtumikia na kumoigia debe kigogo Majoka.
 •  Ni mkware-Anapata sabuni ya kupika keki kwa kuishiriki uroda na Ngurumo.
 • Ni mlevi-Anashiriki katika ulevi pale Mangweni.
 • Ni gwiji wa kejeli-Anatunga nyimbo nyingi za kuwakejeli Tunu na Sidi.
 • Ni mgema-Anashiriki katika harakati za kutengeneza pombe haramu amabayo inawadhuru wanajamii.
 • Ni mwenye majuto-Anaishia kujuta matendo yake aliyoyatenda .“Wamenimaliza ……wamenigeuka .Pombe yote wameimwanga !Nilijua ninawaponza nilijua ninawapunja nilijua ninawadhuru wanasogomoyo lakini nilimezwa na tama .Najuta zaidi ya kujuta .Naomba msamaha ,Tuna ,naomba radhi wanasogamoyo.Naomba ulinzi wenu .Wananiwinda ,”maneno ya mamapima(uk.92)

Umuhimu wake

 • Ni kielezo cha wanajamii ambao hawajali maslahi ya wengine na wanafanya chochote kupata pesa bila kujali wengine .Hana utu.

HUSDA

 • Ni bibiye Majoka
 • Ni mamake Ngao Junior

Sifa zake

 •  Ni mkali-Anamkasirikia Ashua anapomfumania ofisini mwa Bwanake Majoka.
 •  Ni mrembo-Anapenda kujipondoa na kuvaa mavazi ya kuvutia
 •  Ni mwenye jicho la nje-Anamtamani chopi wakiwa pale Majoka and Majoka resort (Husda anarejea .Anapomwona chopi anatembea kwa madaha .Amevaa nguo zilizombana na viatu vyenye vichuchumio virefu.Uso wake umejaa vipodozi .Angali ana miwani myeusi .Anamtazama Chopi kwa macho ya uchu kasha anakaa kando ya Majoka ) (uk 70)
 •  Ni mwenye tamaAnaingia katika ndoa na Bwana Majoka ,si kwa sababu anampenda ila ni kwa sababu ya mali.
 • “Nyanya tafadhali Husda hanipendi ,anapenda mali zangu .Hayo sio mapendo ya dhati .”Maneno ya Majoka (uk 75).

Umuhimu wake

 •  Ni kielelezo cha wanawake wanaoingia katika ndoa kwa sababu ya mali bali si upendo.
 •  Pia anawakilisha baadhi ya wanawake wa viongozi na changamoto wanazozipitia katika ndoa zao.

 CHOPI.

 • Ni tarishi na mlinzi wa Majoka.

Sifa zake

 • Ni kikaraguzi-Anamtumikia Majoka na kummundumia bila kuuliza swali lolote.
 •  Ni msiri-Anaziifadhi siri za Majoka.
 • NI mwenye bidii]-Anafaya kazi yake ya utarishi kwa bidii mno.
 •  Ni mvumilivu-Anavumilia upyoro na ukali wa Bwana Majoka anapomuundumia
 • Ni mpyoro-Anamzungumzia Sudi vibaya anapompeleka kumwona Ashua jela alikofungiwa na Bw Majoka.
 • “Toka nisikutoe ,shamba likikushida kulima sema.”(uk 50)
 • “Hamjamaliza kupigana Kisi?”Muda wenu umekwisha nian kazi ya kufanya.” (uk 50)

Umuhimu wake

 •  Ni kielekezo cha watu wanawatumikia viongozi bila kuuliza maswali.
 •  Pia ni kielelezo cha walinzi katili

HASHIMA

 • Ni mamake Tunu

Sifa zake

 • Ni mwenye mapenzi ya dhati-Anapenda mwanawe Tunu kwa dhati na kumshughulikia sana katika hali yake ya ulemavu.
 • Ni jasiri-Amevumila mateso mengi kutoka kifo cha bwanake hadi kulemazwa kwa mwanawe Tunu.
 • Ni mwenye bidii-Amevuna mchele mwingi jambo linaloashiria bidii yake shambani.
 • Mwenye utu-Alikubali kuwatunza Pili na Pendo walipotumwa kwake na Tunu.

Umuhimu wake

 • Ni kielelezo cha kina mama wenye utu na wenye mapenzi ya dhati kwa wanao.
 •  Pia ni kielelezo cha kina mama wanaojua uchungu wa kupoteza waume wao kwa sababu ya uongozi mbaya.

 KINGI

 •  Ni mkuu wa polisi.

Sifa zake

 • Ni mwenye bidii-Anafanya kazi yake kwa bidii mno.
 • Ni mkakamavu-Anakataa kufuata amri za Majoka na kuwafuata wananchi
 • Anamkabili Bw Majoka moja kwa moja bila woga hata anapatishiwa kuachishwa kazi.
 •  Ni mwenye utu-Anajali haki za msingi za wanachi na kuwalinda wakati wanapoandamana.

Umuhimu wake

 •  Ni kielelezo cha polisi wachache weny utu na wanaolinda haki za kimsingi za wananchi.

 BABU

 • Ni mhusika kiepiki
 •  Ni babu yake B.w Majoka.

Sifa zake

 •  Ni mhusika kiepiki-Anatokea ndotoni.
 •  Ni mkweli-Anaisuta nafsi ya Majoka kwa kumweleza mambo kinagaubaga.
 • Ni mwenye utu-Anajaribu kumzidua na kumuonyesha Majoka umuhimu wa kuwa na utu.
 • Ni mwenye busara-Anatumia maneno yaliyojawa busara kuisuta nafsi ya Majoka.

Umuhimu wake

 • Ametumiwa kudhihirisha utamaduni wa kiafrica unaoshikilia kuwa kuna uhai baada ya kifo na kuwa matendo yetu huwaadhiri waliokufu
 •  Ametumiwa kusuta uongozi mbaya unaondelezwa na viongozi wngi duniani.

 DAKTARI

 •  Ni daktari wa Majoka.

Sifa zake

 •  Ni mwenye bidii-Anatekeleza wajibu wake wa daktari kwa bidii mno na kumuhudumia Bw Majoka kwa njia inayofaa.
 • Ni mwenye busara-Anapogundua kuwa Majoka anazungumza na babu yake anaiga ile nafasi ya babu moja kwa moja.
 • Ni mwenyee utu-Anajaribu kumtuliza Majoka na kupima maneno yake asiye akamuumiza Husda mke wake .

Umuhimu wake.

 •  Ni kielelzo cha wafanyikazi wanaowajibika katika kutimiza jukumu lao.

NESI.

 • Ni muuguzi wa Majoka.

Umuhimu wake.

 •  Ametumiwa kumjenga daktari na kudhihirisha umuhimu.

MTU 1 NA MTU 11

 •  Ni mlvi-Wanalewa pale Magweni pa Mama Pima.

Umuhimu wao.

 •  Wametumiwa kumjenga mhusika Ngurumo na kumkejeli Sudi na Tunu

PILI NA PENDO

 • Ni watoto wa Ashua na Sudi.
 • Wametumia kudhihirisha changamoto wanazozipitia Sudi na Ashua.

 MWANGO

 • Ni askari katika makazi ya Majoka.

Sifa zake

 •  Ni kikaragozi-Anamtumikia Majoka bila kuuliza maswali.

Umuhimu wake .

 •  Ni kielelezo cha askari wanaowatumikia viongozi wabaya na kuendeleza uongozi wao dhalimu.

 MJUMBE

 • Ni mtangazaji katika sauti ya mashujaa.
 • Ametumiwa kuendeleza uongozi dhalimu na ukoloni mamboleo.
Total Execution Time content: 0.00038026571273804 Mins Total Execution Time social : 0.0001 Mins

Read Next

Total Execution Time red next: 0.0000 Mins

Search Now


Categories