Vitendawili vya kiswahili na majibu yake - answers

17 min read

Vitendawili vya kiswahili na majibu yake

A
1.  Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi
2.  Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono
3. Afuma hana mshale. Nungunungu
4. Ajenga ingawa hana mikono. Ndege
5. Ajifungua na kujifunika. Mwavuli
6. Akitokea watu wote humwona. Jua
7. Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa
8. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba
9. Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu
10. Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi
11. Aliwa, yuala; ala, aliwa. Papa
12. Amchukuapo hamrudishi. Kaburi
13. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi. Giza
14. Amefunua jicho jekundu. Jua
15. Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri. Mbegu
16. Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa
17. Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba
18. Amekula ncha mbili. Wali
19. Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe. Kaburi
20. Anakuangalia tu wala halali au kutembea. Picha
21. Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba. Mchanga
22. Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele. Ardhi
23. Anakula lakini hashibi. Mauti
24. Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana. Moto
25. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’. Kitanda
26. Ashona mikeka wala hailali. Maboga
27. Askari wangu wote wamevaa kofia upande. Majani
28. Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi. Chunguchungu
29. Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili. Fedha
30. Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti. Mvua
31. Atolewapo nje hufa. Samaki
B
32. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa
33. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi
34. Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu
35. Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi
36. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa
37. Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua
38. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka
39. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu
40. Bak bandika, bak bandua. Nyayo
41. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango
42. Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho
43. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia

C
44. Chakula kikuu cha mtoto. Usingizi
45. Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani. Nyama na mfupa
46. Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi. Jua
47. Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja. Mwezi/Jua
48. Cheupe chavunjika manjano yatokea. Yai
49. Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia
50. Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya
51. Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu

D
52. Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo
53. Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni
54. Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui
55. Dume wangu amelilia machungani. Radi

F
56. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani
57. Fika umwone umpendaye. Kioo
58. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini
59. Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa

H
60. Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua
61. Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo. Maji
62. Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea. Nywele
63. Hakionekani wala hakishikiki. Hewa
64. Hakisimami, na kikisimama msiba. Moyo
65. Hakuchi wala hakuchwi. Kula
66. Halemewi wala hachoki kubeba. Ardhi
67. Hamwogopi mtu yeyote. Njaa
68. Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua. Ukucha
69. Haoni kinyaa. Mvua
70. Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu. Mvua
71. Hasemi, na akisema hatasahaulika. Kalamu
72. Hasimamishwi akiwa na ghadhabu. Upepo
73. Hata inyeshe namna gani haifiki humu. Kwapani
74. Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto. Pua ya mbwa
75. Hata Mzungu ameshindwa. Mauti
76. Hauchagui chifu wala jumbe. Utelezi
77. Hausimiki hausimami. Mkufu
78. Hawa wanaingia hawa wanatoka. Nyuki mzingani
79. Hesabu haihesabiki. Nyota
80. Huitumia kila siku lakini haiishi. Miguu
81. Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu. Jua
82. Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! Mkia wa kondoo
83. Hula lakini hashibi. Sindano
84. Hulala tulalapo, huamka tuamkapo. Jua
85. Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue. Matendegu ya kitanda
86. Huna macho lakini wakamata wanyama. Ndoana
87. Hupanda mtini na mwenye kichaa wake. Kivuli
88. Hutembea watatu. Mafiga
89. Hutoka upesi sana lakini hasalimu. Kuku
90. Huwafanya watu wote walie. Moshi
91. Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi. Chungu jikoni
92. Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi. Mbegu na matunda

I
93. Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka. Herufi "K"
94. Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali. Kifo

J
95. Jembe la Wangoni haliishi. Miguu/Nyayo
96. Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? Nywele kichwani
97. Jiwe litoalo maji. Macho

K
98. Kaburi la mfalme lina milango miwili. Kata ya kuchukulia Maji kichwani
99. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma. Paka na mkia wake
100. Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote. Kizingiti cha mlango
101. Kama unapenda, mbona usile? Ulimi
102. Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa nikautumia. Nazi
103. Kapanda mti pamoja na uchawi wake. Tumbaku inaponuswa puani
104. Kidimbwi kimezungukwa na majani. Macho
105. Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa. Maziwa
106. Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele. Mvua
107. Kila mtu atapitia malango huo. Kifo
108. Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita. Mlango
109. Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni. Jua
110. Kileee! Hiki hapa. Kivuli
111. Kilimsimamisha chifu njiani. Chawa
112. Kina mikono na uso lakini hakina uhai. Saa
113. Kinaniita lakini sikioni. Mwangwi
114. Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji. Taa ya utambi
115. Kisima kidogo kimejaa changarawe. Kinywa na meno
116. Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi. Mimba
117. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Moto
118. Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe. Kuku aatamiapo mayai
119. Kiti nyikani. Uyoga
120. Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu. Maisha ya binadamu
121. Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu. Kipara
122. Kombe ya Sultani Ii wazi. Kisima
123. Kondoo wangu amezaa kwa paja. Mhindi
124. Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima. Konokono
125. Kondoo za mtoto zamaliza mavuno. Jiwe la kusagia
126. Kufanya kwa ridhaa mojamoja. Kusuka mkeka
127. Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege. Nyoka au samaki
128. Kuku wangu amezalia miibani. Nanasi au chungwa
129. Kuku wetu hutagia mayai mikiani. Matunda
130. Kuna mlima mmoja usio pandika. Nafasi kati mdomo na pua
131. Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje. Ghala
132. Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi. Chongo
133. Kunguru akilia hulilia mirambo. Mtoto akililia maziwa
134. Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili. Watoto wa ng'ombe na mbuzi
135. Kwetu mishale na kwenu mishale. Mikia ya panya
136. Kwetu twalala tumesimama. Nguzo za nyumba

L
137. La mgambo limelia wakatoka weusi tu. Chunguchungu
138. Likienda hulia, likirudi halilii. Debe aka buyu
139. Likitoka halirudi. Neno
140. Liwali amekonda lakini hana mgaga. Sindano


M
141. Mama ametengeneza chakula lakini hakula. Chungu cha kupikia
142. Mbona kinakumeza lakini hakikuli? Nyumba
143. Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? Mafiga
144. Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? Katani
145. Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’. Mlango
146. Mdogo lakini humaliza gogo. Mchwa
147. Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye
 hatukuitambulisha tena. Kohozi
148. Mfalme hushuka kwa kelele. Mvua
149. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni. Moto na mafiga
150. Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza. Hindi
151. Mhuni wa ulimwengu. Inzi
152. Mkanda mrefu wafka mpaka pwani. Njia
153. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi
154. Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa
155. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali
156. Mlimani sipandi. Maji
157. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo
158. Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima
159. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe
160. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake
161. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi
162. Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba
163. Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio
164. Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu
165. Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka
166. Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni
167. Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo
168. Mvua hema na jua hema. Kobe
169. Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe
170. Mwadhani naenda lakini siendi. Jua
171. Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi
172. Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru
173. Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki
174. Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka
175. Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani
176. Mwezi wangu umepasuka. Kweme
177. Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua
178. Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua
179. Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu
180. Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi

N
181. Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia. Mwiba
182. Nakikimbilia lakini sikikuti. Njia
183. Nakupa lakini mbona huachi kudai. Tumbo
184. Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185. Nameza lakini sishibi. Mate
186. Namkimbiza lakini simkuti. Kivuli
187. Namlalia lakini halii. Kitanda
188. Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa. Kigino
189. Nanywa supu na nyama naitupa. Muwa
190. Napigwa na mvua na nyumba ipo. Matunda ya pua/Kwapa
191. Natembea juu ya miiba lakini hainichomi. Miiba
192. Natembea juu ya miiba lakini sichomwi. Ulimi
193. Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni. Mbwa
194. Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana. Mzinga was nyuki kwa nje
195. Natengeneza mbono lakini alama hazionekani. Mzinga wa nyuki
196. Ndege wengi baharini. Nyota
197. Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani. Macho
198. Ngoja nikumbuke. Boga changa
199. Ng’ombe wa baba watelemka mtoni. Mawe mtoni
200. Ng’ombe wa babu huchezea miambani. Mijusi
201. Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii. Vbuyu
202. Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.Viazi vitamu udongoni
203. Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu. Pesa/Nyayo
204. Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni. Katani
205. Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja. Fimbo ya kuchunga
206. Ngozi ndani nyama juu. Firigisi
207. Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa. Nyusi
208. Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna. Kioo
209. Nikienda arudi, nikirudi aenda. Kivuli majini
210. Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’. Mwangwi
211. Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo
212. Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai
213. Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa
214. Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi
215. Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka
216. Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi
217. Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli
218. Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo
219. Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho
220. Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua
221. Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga
222. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani
223. Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu
224. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko
225. Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba
226. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu
227. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu
228. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele
229. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki
230. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
 kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
 walikwenda Rumi? Hakuna
231. Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani
232. Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura
233. Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli
234. Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia
235. Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio
236. Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi
237. Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu
238. Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige
239. Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga
240. Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli
241. Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa. Mgomba
242. Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja. Kuangua tunda Ana nazi
243. Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki. Mtego
244. Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto. Kivuli
245. Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani. Moto
246. Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba. Dirisha Ana ufa
247. Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia. Kata
248. Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani. Mimba
249. Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni. Nyota
250. Nimezaliwa na mguu mmoja. Uyoga
251. Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi. Ulimi na meno
252. Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu. Maisha
253. Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi. Jina
254. Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua. Dada
255. Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima. Mke
256. Nina mwezi ndani ya bakuli. Maziwa
257. Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani. Jembe
258. Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa. Mdomo
259. Nina pango langu lilojaa mawe. Kinywa
260. Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe. Kunguru
261. Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki. Mafiga
262. Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi. Kivuli
263. Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi. Jiwe
264. Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi. Maji na mkojo
265. Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi. Chungu cha kupikia
266. Ninakwenda naye na kurudi naye. Kivuli
267. Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu. Kichwa
268. Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu. Jua au mwezi
269. Njia yapitwa siku zote lakini haina alama. Njia ya jua au mwezi
270. Njoo hapa nije hapo. Kiraka
271. Nne nne mpaka pwani. Matendegu
272. Nusu mfu nusu hai. Sungura alalapo
273. Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe. Kinoo
274. Nyama ya Reale haijai kikombe. Mkufu
275. Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo. Kitanda
276. Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja. Mwembe
277. Nyumba yangu ina milango mingi. Kichuguu
278. Nyumba yangu ina nguzo moja. Uyoga
279. Nyumba yangu kubwa, haina mlango. Yai
280. Nyumba yangu kubwa, haina taa. Kaburi
281. Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni. Konokono

O
282. Oh! Mwanamke aliyevunja chungu mshangao wake
283. Ondoka nikae. Maji ya mfereji

P
284. Paa alipenga hata pua ikapasuka. Mbarika
285. Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa? Was kwanza in Mtoto tumboni mwa mamake, was pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, was tatu ni mama mwenyewe
286. Panda ngazi polepole. Sima ya ugali
287. Para hata Maka. Utelezi
288. Pete ya mfalme ina tundu katikati. Kata ya kuchukulia mizigo
289. Poopoo mbili zavuka mto. Macho
290. Po pote niendako anifuata. Kivuli

R
291. Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga
292. Reli yangu hutandika ardhini. Siafu
293. Ruka Riba. Maiti

S
294. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani
295. Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole
296. Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia
297. Sijui aendako wala atokako. Upepo
298. Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini
299. Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu
300. Subiri kidogo! Miiba
301. Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa. Maji

T
302. Taa ya bure. Jua au mwezi
303. Taa ya Mwarabu inapepea. Kilemba
304. Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa. Makamasi
305. Tandika kitanga tule kunazi. Nyota
306. Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia. Mkufu
307. Tatarata mpaka ng’ambo ya mto. Utando wa baibui
308. Tatu tatu mpaka pwani. Mafiga
309. Tega nikutegue. Mwiba
310. Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke. Mahindi ama yai
311. Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania. Mbono
312. Tonge la ugali lanifikisha pwani. Jicho
313. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika. Maji
314. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu. Kucha
315. Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata. Kinoo
316. Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa. Mbingu na nchi
317. Tumvike mwanamke huyu nguo. Kuezeka nyumba
318. Tunajengajenga matiti juu. Mapapai
319. Twamsikia lakini hatumwoni. Sauti

U
320. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba. Mwangwi
321. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia. Fisi
322. Ukimwona anakuona. Jua
323. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto. Kinyonga
324. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo. Mwamba
325. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki. Moshi
326. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini. Tundu LA sindano
327. Ukoo wa liwali hauna haya. Wanyama
328. Ule usile mamoja. Kifo
329. Umempiga sungura akatoa unga. Funds LA mbuyu
330. Unatembea naye wote umjiao atakuona. Bakora
331. Upande wote umjiao atakuona. Kinyonga
332. Ushuru wa njia wKujikwaa Kujikwaa
333. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu. Nywele

V
334. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki. Moto

W
335. Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme
336. Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua
338. Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba
339. Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga
340. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango
341. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota
342. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo
343. Wanastarehe darini. Panya
344. Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho
345. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga
346. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu
347. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo
348. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu
349. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
350. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi
351. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto
352. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
 haonekani tena. Kivuli
353. Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali
354. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme

Wazee wawili wanashuka mlima - nyayo

Y
355. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia

Z
356. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto
357. Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni
358. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto


Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu___
2. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu ____
3. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi ____
4. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? ____
5. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu ___
6. Watu wamehama Askari wekundu wakazidi nyikani ___
AINA ZA KOFIA MBALIMBALI Kofia ni vazi lililoshonwa livaliwalo kichwani.
Hizi ndizo aina mbalimbali za Kofia;
1. Shumburere ni kubwa na pana ambayo hufumwa au husukwa kwa ukindu au miyaa.
2. Tarbushi / Tarabushi / Kitunga ni kofia ya rangi,hasa nyekundu,yenye shada la nyuzi ndefu nyeusi. Katika kipindi cha Mother In-Law,kofia hii huvaliwa na Mustafa.
3. Topi ni aina ya kofia isiyokuwa na chepeo
4. Pama ni aina ya kofia yenye ukingo mpana
5. Mdongea ni kofia nyeupe inayoshonwa kwa cherehani.
6. Kibapara ni kofia kuukuu
7. Kidotia ni inagovakiwa na mtoto kwa minajili ya kumkinga dhidi ya baridi.
8. Helmeti / Huda ni kofia ya chuma au plastiki ya kukingia kichwa kisidhuriwe na pigo lolote na upepo dhidi ya kichwa.
9. Hudi ni aina ya kofia inayoshonewa kwenye nguo kama vile; Jaketi,fulana/sweta,Umbopa,Bwelasuti na 'Jampa.'
10. Dusumali / Ushungi ni kilemba cha kitambaa cha rangirangi kibachovaliwa na wanawake(Hii si aina ya kofia)
11. Kilemba ni kitambaa au nguo iliyozungushwa kichwani kama vile washiriki wa dhehebu la 'Korino' na wahindi Kalasinga(hii si aina ya kofia tafadhali)
12. Chepeo ni aina kofia yenye ukingo wa nusuduara uliotokeza mbele inayoshonwa kwa kitambaa cha nguo,turubai,sandarusi,n.k
13. Bulibuli ni mfumo wa kofia nyeupe ya mwambao wa Pwani ya Afrika Mashariki iliyotiwa nakshi; kofia ya Kazi.
14. Boshori hii ni aina ya kofia iliyofumwa kwa sufu,hasa huvaliwa wakati wa baridi. Hii ndiyo ile huitwa Marvin katika lugha ya kawaida. Pia kuna wale hutohoa na kuiita Mavini .
15. Baraghasia ni aina ya kofia ya mviringo iliyofumiwa mapambo ya maua.

Fahamu haya tafadhali;
a). Ukingo sehemu ya mbele ya kofia inayozuia jua kufikia macho.
b). Kahafi ni sehemu ya juu ya kofia ,paa la kofia
Kama kuna ile sijaiangazia ilhali unaifahamu,naomba utujulishe. Kichango Kuchangizana huku nikiwa na imani kama imamu kuwa hakuna ziada mbovu!
Bibi wa Mfalme hunivaa Nini kichwani

vitendawili and answers

 

vitendawili na majibu grade 3

 

vitendawili grade 5

 

vitendawili na majibu grade 4

 

vitendawili na majibu grade 6

 

kamusi ya vitendawili online

 

buli buli ni nini

 

shimizi ni nini

 

bwelasuti ni nini

nyumba yangu inasimama na mguu moja

Ukumbuu wa babu ni mrefu -barabara/ njia

tarbushi

 

umuhimu wa mavazi ya kinga

 

 
Kamusi Teule ya Kiswahili. Kilele cha Lugha
(Swahili Edition) by Ahmed E. Ndalu, Hamisi Babusa, Suleiman A. Mirikau
Paperback, 804 Pages, Published 2013 by East African Educational Publishers
ISBN-13: 978-9966-25-936-3, ISBN: 9966-25-936-8

Kamusi Angaza Msingi. kwa shule za
(Swahili Edition) by Ahmed E. Ndalu
Paperback, 384 Pages, Published 2011 by East African Educational Publishers
ISBN-13: 978-9966-25-808-3, ISBN: 9966-25-808-6

Pendo la Halineshi by Ahmed E. Ndalu, Hamisi Chombo
113 Pages, Published 2015
ISBN-13: 978-9966-47-880-1, ISBN: 9966-47-880-9

Mazoezi na Marudio Kwa Vyuo Vya Walimu by Ahmed E.Ndalu
Published by East African Publishers
ISBN-13: 978-9966-46-918-2, ISBN: 9966-46-918-4

Beyond expectations
from charcoal to gold by Ahmed E. Ndalu
ISBN-13: 978-978-996-625-7, ISBN: 978-996-625-3

Masomo ya Kiswahili sanifu
Kitabu cha mwanafunzi. Kidato cha 2 by Ahmed E. Ndalu
137 Pages, Published 2016
ISBN-13: 978-9966-34-992-7, ISBN: 9966-34-992-8

Kamusi ya Semi za Kiswahili by Kitula G. King'ei, Ahmed E. Ndalu
Paperback, 139 Pages, Published 2003 by East African Educational Publishers
ISBN-13: 978-9966-46-540-5, ISBN: 9966-46-540-5

Kamusi Yangu Ya Kwanza by Ahmed E. Ndalu
194 Pages, Published 2000 by East African Publishers
ISBN-13: 978-9966-25-008-7, ISBN: 9966-25-008-5

Mwangaza wa Kiswahili
(Swahili Edition) by Ahmed E. Ndalu
174 Pages, Published 1997 by East African Educational Publishers
ISBN-13: 978-9966-46-013-4, ISBN: 9966-46-013-6

Kamusi ya vitendawili na mafumbo by Ahmed E. Ndalu, Henrietta M. Ikambili
111 Pages, Published 1991
ISBN-13: 978-9966-46-712-6, ISBN: 9966-46-712-2

Hadithi njoo by Ahmed E. Ndalu
28 Pages, Published 1990
ISBN-13: 978-9966-919-34-2, ISBN: 9966-919-34-1

Hadithi njoo by Ahmed E. Ndalu
38 Pages, Published 1990
ISBN-13: 978-9966-919-33-5, ISBN: 9966-919-33-3

Kamusi ya methali za Kiswahili
(Swahili Edition) by Kitula G. King'ei, Ahmed E. Ndalu
Paperback, 206 Pages, Published 1989 by Heinemann Kenya
ISBN-13: 978-9966-46-446-0, ISBN: 9966-46-446-8

Total Execution Time content: 0.00038763284683228 Mins Total Execution Time social : 0.0001 Mins

Read Next

Total Execution Time red next: 0.0000 Mins

Search Now


Categories