Mwongozo Wa Kigogo – Uchambuzi wa Tamthilia ya Kigogo Pdf Notes Download online
3 min read
Description
ANWANI YA TAMTHILIA.
Kigogo ni mtu mwenye madaraka makubwa kiutawala.
Majoka anatumia madaraka yake kulaghai wananchi, anachukua vilivyo vyao.
Anatangaza kipindi cha mwezi mzima cha kusheherekea uhuru kutumia madaraka aliyonayo.
Majoka anafunga soko la Chapakazi ili sehemu hiyo ajenge hoteli ya kifahari kwa kutumia madaraka aliyonayo.
Anapandisha bei ya chakula katika kioski kwa vile ana madaraka.
Majoka anatumia mamlaka yake kumteka na kumtia ndani Ashua.Anamtendea ukatili, Ashua ana majeraha kutokana na kichapo.
Majoka anapanga kifo cha Jabali, mpinzani wake. Anampangia ajali na kuangamiza wapinzani wake pamoja na chama chake kwa kutumia mamlaka yake..
Majoka anapanga kutumia mamlaka yake kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu kifo cha Jabali.
Kigogo – Maudhui
Baadhi ya maudhui yanayojitokeza kwenye tamthilia hii ni kama vile:
1. Uongozi mbaya ambao unadhihirika kupitia kwa Majoka kulifunga soko la Chapakazi kwa madai kuwa Ni chafu, kumbe ilikuwa Ni njama ya kuinyakua ardhi hiyo.
– Uongozi wake unafungulia Biashara ya ukatajo miti, Jambo linalosababisha ukame.
– uongozi wake unampa Mama pima kibali Cha kuuza pombe haramu inayowua na kuwapofusha vijana.
– Anatumia hela mikopo kwenye miradi isiyokuwa na manufaa kwa Wanasagamoyo kv; kuchonga kinyago.
– anawauzia wanafunzi dawa za kulevya “sumu ya nyoka’ Jambo linawafanya kutofuzu, wanakuwa makabeji.
– Anawaua wapinzani wake kama vile Jabali.
– Anaifunga runinga ya Mzalendo kwa kupeperusha maandamano ya kina Tunu.
2. Ujinga
– Anatangaza kipindi cha mwezi mzima wa Mapumziko.
– Uongozi wake unajivunia kuwa na kampuni kubwa ya kutengeneza sumu ya nyoka barani Afrika. dawa hizo zinamuua mwanaye Ngao Junior.
– Asiya anamgawia ngurumo uroda ili amsaidie kupata kandarasi ya kuoka keki ya Uhuru.
– Majoka anawaita wanasagamoyo wajinga.
– Boza na Kombe wanaparamia masazo ya keki ya Uhuru bila kutambua kuwa ilikuwa imeliwa kwingine.
– Mama pima anawauzia wenzake pombe haramu inayowaua na kuwapofusha.
3. Ufisadi
– Majoka anainyakua ardhi ya soko la Chapakazi na kumtengea Kenga kipande.
– Majoka anataka Ashua amhonge kwa uroda ndipo amsaidie chakula.
– Uongozi wa Majoka unawanunulia vijana pombe ili kuunga mkono.
– Mama pima anamhonga Ngurumo leave uroda ili amsaidie kupata kandarasi ya kuoka keki ya Uhuru.
– Mshauri mkuu wa Majoka, Kenga Ni binamu yake.
4. Ukatili
– Majoka anamuua Jabali mpinzane wake wa awali.
Majoka anamfungia Ashua kwa madai ya kuzua fujo kwenye ofosi ya umma.
-Majoka analifunga soko la Chapakazi lililokuwa likitegemewa na Wanasagamoyo.
– Majoka anaeatuma majambazi kumuua Tunu, lakini wanaishia kumvunja tu mguu.
– Majoka anaamuru Askari kuwafyatulia waandamanaji risasi na kuwaua.
– Baada ya kulifunga soko Majoka anapandisha Bei ya chakula maradufu katika kioski Cha kampuni yake.
Yapo mengi kama vile: usaliti, nafasi ya mwanamke, nafasi ya vijana, ulevi, umaskini, ukiukaji wa haki, elimu, ukabila miongoni mwa mengine mengi. Jihisi huru kuyajadili hapa…
NAFASI YA MWANAMKE
1. Mwanamke ni katili-
Mamapima anawauzia wanasagamoyo wenzake pombe haramu inayowaua na kuwapofusha Wengine.
2. Mwanamke ni mwenye mapinduzi
Tunu anaongoza harakati za mapinduzi dhidi ya Uongozi dhalimu wa Majoka kwa ushirikiano wa Sudi.
3. Mwanamke ni msomi
Tunu Ana shahada na uanasheria inayomwezesha kutetea haki za Wanasagamoyo dhidi ya Uongozi dhalimu wa Majoka.
Ashua pia Ana shahada ya ualimu lakini anauza maembe sokoni Licha ya kupewa kazi kwenye shule za Majoka and Majoka Academy anazodai Ni za kihuni.
4. Mwanamke ni Jasiri
Licha ya kuvunjwa mguu, Tunu anaendeleza mapinduzi Hadi anafanikiwa kumwondoa Majoka mamlakani.
Pia anafahamu ukatili wa Majoka lakini anamweleza waziwazi kuwa watalipa kila tone la damu walilomwaga Sagamoyo.
5. Mwanamke ni mwenye wivu
Husda anapigana na Ashua ofisini mwa Majoka akidai kuwa amekuja kumnyanganya mume.
6. Mwanamke ni Mwasherati
Mamapima anamgawia ngurumo uroda ili amsaidie kupata kandarasi ya kuoka keki ya Uhuru
7. Mwanamke ni Mwenye uchu
Husda anapomwona Chopi, anaanza kutembea kwa maringo huku akionyesha macho ya uchu.
TUENDELEZE MJADALA…. ZIPO TELE
mwongozo wa kigogo pdf
kigogo notes
kigogo summary
riwaya ya kigogo
kigogo riwaya
kigogo summary notes
uchambuzi wa kigogo
mwongozo wa kigogo pdf download
Total Execution Time content: 0.000675102074941 Mins
Total Execution Time social : 0.0001 Mins