1. Saidi : Hallo…………Hallo….Huyo ni Bw. Mohamed?
Mohamed : Ndio…uko wapi…
Saidi : Shuleni…sasa…ulinifikishia ujumbe?
Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwa
Saidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.
Mohamed : Sina pia, nitatuma sms
Saidi : Iwe saa hii eh?
Mohamed : Baada ya dakika tano
Saidi : Good day
Mohamed : Welcome
(a) Taja na uthibitishe sifa zinazojitokeza katika mazungumzo haya
(b) Eleza sababu za wazungumzaji kutumiambinu zifuatazo katika mazungumzo yao
(i) Mdokezo
(ii) Lugha mseto
2 . Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.
3. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:-
Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini iwapo nyingi mwilini hugeuzwa kuwa glukosi ambayo huhifadhiwa mwilini. Hii huwa msingi wa unene pia ambao unahatarisha afya. Jamaa yake aliyeaga dunia alikuwa mgonjwa wa bolisukari ambayo inaweza kurithishwa. Kimsingi, lazima awe na welewa bora kabisa wa lishe. Mwenzake naye aliathiriwa na aflatoxins zilikuwa kwenye chakula alichokula.
(a) Sajili hii inapatikana wapi? Kwa nini?
(b) Taja sifa zinazohusishwa na sajili yenyewe
4. Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya
5 (a) Ni mambo yapi yanayochangia kudidimia kwa Kiswahili nchini Kenya.
(b) Mambo haya yanaweza tatuliwa vipi?
6. a) Bainisha kwa kutoa mifano sifa tano za lugha ya vijana ‘sheng’
b) Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili
7.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:-
Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo,
mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni gold !
Hiyo siyo real life maze ! Round hii maze ni ”Ku-chill!” Usipige ma-stunts zingine
zitakuacha uki-regret later! NI POA KU- CHILL au aje maze?
a) Bainisha rejista ya mazungumzo haya
b) Kwa kurejelea kifungu andika sifa za rejista hii.
c) Kwa nini watu hutumia lugha zaidi ya moja.
d) Orodhesha hatua tatu zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo yanayokumba
Kiswahili nchini.
8. Soma mzungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :
A : Ohh, dada Naomi
B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
A: Asifiwe sana
B: Ehh dadangu, miezi …mingi…sijakuona
A: dada wee…Nilitumwa huko kusini …Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata…
B: Ehh, usiwe kama Yona
A: Habari ya siku nyingi?
B Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
A: Amen!
B: Nimeendelea kuiona neema yake
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Halleluya
A: Ni Mungu wa miujiza!
B : Amen. Hata nami nimeona neema yake
Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
A : Amen !
B : Ni Mungu wa ajabu kweli !
A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana
ameshindwa
B : Ameshindwa kabisa
Maswali:-
(i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua
(ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii
(iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili
Afrika mashariki na kati
9. Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na
mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya….
(a) Hii ni sajili gani?
(b) Eleza sifa za mazungumzo ya sajili hii
10. Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili
11.` (a) Fafanua sifa za matumizi ya lugha katika muktadha wa maabadini
(b) Matumizi ya lugha yoyote ile huthibitiwa na mambo fulani. Fafanua matano kati ya hayo
12. AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!
SHIKU : Namba nane ngapi?
AZIZ : Mbao ingia, blue.
SHIKU : Nina hashuu.
AZIZ : Blue Auntie.
SHIKU : Sina.
AZIZ : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba.
AHENDERA : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi.
AZIZ : Dinga inakunywanga petrol mzee.
AHENDERA: Kumi mingi.
AZIZ : Haaya ingia twende. Driver imeshon twende.
Maswali
(i) Eleza muktadha wa mazungumzo haya
(ii) Taja sifa sita za lugha iliyotumika katika mazungumzo haya
13. Kifuatacho ni kifungu kifupi cha mazungumzo. Kisome kisha ujibu maswali yaliyoulizwa:-
Mzee Oluoch :…………………………………………………………..ni kweli hayo!
Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu.
Mzee Oluoch : Na wangu amehitimu na sasa ana shahada ya uzamili. Yeye ni mhandisi
mkuu. Chukua tu mbuzi hamsini na utukubalie kujenga uhusiano wa ukwe.
Mzee Mwenda : Je, mbuzi hao ni wa ‘mfuko’ au ni …….?
Mzee Oluoch : Kuna wa mfuko ……thelathini na hao wengine ishirini.
Mzee Mwenda : Basi lete hao ulio nao. Wengine hamsini watabaki deni. Utakuwa
ukinilipa polepole. Idhini yangu nimetoa ili mipango iendelee.
(a) Mazungumzo ya aina hii hutokea katika muktadha wa aina gani?
(b) Eleza sifa nane za lugha inayotumika katika wa aina hii
1. (a) – Lugha elezi imeumika
– lugha takriri
-Lugha mseto hutumika
– Serntensi fupi fupi hutumika
-Kanuni za lugha hazizingatiwi
– Huendesha kwa malumbano na ngonjera (hoja 6×1=al. 6)
(b) (i) Mazungumzo hulipiwa – kupunguza gharama kupoteza mda (hoja 2×1=al. 2)
(ii) Uhusiano wao wa kielimu
2. Ushindani kutoka lugha nyingine kama kiingereza
Lugha imetengwa katika matumizi ofisini za kiserikali
3. a) hospitalini/ uwanja kisayansi
b) Sifa za sajili ya hospitalini Matumizi ya msamiati maalum
Matumizi ya vifupisho ambavyo vinaeleweka na wanaohusika na uwanja wenyewe
Kuwepo kwa maelezo yanayoambatanishwa na michoro kujaliza maelezo yanayotolewa
Matumizi ya alama zinazohusishwa na taaluma ya hisabati hasa katika maagizo ya
kutumia dawa
Huweza kuwepo na matumizi ya maneno ya kilatini yanayohusishwa kwa kiasi kikubwa
na taaluma hii
Huweza kutumia neno mgonjwa kumweelezea mtu badala ya jina k.m yule mgonjwa wa
homa ameruhusiwa kwenda nyumbani
Utohozi wa maneno hutumika
Kuna kuchanganya ndimi
Lugha hii ni ya heshima hasa upande wa mgonjwa
Sarufi huzingatiwa Zozote 7×1=7 Mahojiano kati ya mgonjwa na daktari
4. Mikakati inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Kenya
na maendeleo yake
5. (a)- Matumizi ya sheng’ katika lugha ya Kiswahili
– Kushushwa hadhi ya Kiswahili – Kiswahili kimepewa nafasi finyu ukilinganisha na
Kiingereza
– Vyombo vya habari – vinatumia lugha ya Kiswahili ovyo ovyo bila kuzingatia usanifu wake.
– Ushindani mkubwa ambao Kiswahili kinapata kutoka lugha nyingine k.m. kifaransa, kingereza.
– Kutokuwepo kwa mwongozo na taasisi inayokuza na kuendeleza msamiati na istilahi za Kiswahili.
– Kutokuwepo kwa waandishi wa kutosha wanaoandika katika lugha ya Kiswahili sanifuUGU*
– Ukosefu wa ufadhili wa kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili
– Kutokuwepo kwa sera madhubuti au imara kuhusu matumizi ya Kiswahili sanifu
– Kasumba ya kikoloni miongoni mwa watu
(b) kutilia mkazo ufundishaji ufaao wa kiswahili katika shule na taasisi zote
– Kupitishwa kwa sera nzuri kuhusu Kiswahili, kuhimiza kuwepo kwa idara za Kiswahili
katika taasisi nchini
– Kubuniwa kwa vyombo vya kukiendelza Kiswahili kukisambaza na kuhimiza matumizi yake
– Wachapishaji kuhimizwa kuchapisha kazi za Kiswahili sanifu ili wananchi na wanajamii
kwa jumla kufaidika.
– Kuwepo kwa vipind vya redio na runinga ambavyo vihinamiza matumizi sanifu ya lugha
ya Kiswahili.
– Serikali kutenga fedha kila mwaka ambazo zitachangia katika utafiti na maendeleo ya
Kiswahili
– Kuanzishwa kwa tuzo zitakazopewa waandishi wanaoandika kazi nzuri zinazosaidia
ukuzaji wa kiswahili.
– Kuhimiza uchapishaji wa magazeti mengi ya Kiswahili
6. (a) huchanganya lugha hasa kiswahili na kingereza k.m. utado, anani enjoy.
– Hufupisha maneno k.m. mtoi, tao, Nai , Kach
– Hutumia misimbo k.m. keja, ocha, ndae
– Lugha fiche k.m. ganja (bangi), mapai (polisi)
(b) Mashindano na lugha zingine kama Kingereza.
– Kasumba kwamba lugha ya kiswahili ni duni/ya watu wasiosoma.
-Sura mbov za serikali
-Ukosefu wa taasisis maalum za kuendeleza kiswahili.
-Matumizi ya ‘sheng’ yanadidimiza kiswahili (zozote 5×1=al.5)
7. (a)Lugha ya vijana
(b) •Kubadilisha msimbo –usifikirie kila kitu unaona ni reality.
•Si lugha sanifu-Najua ma-mission ni nyingi lakini jo, mambo imebadilika
•Matumizi ya sheng- Ma-mission
Ku-chill
Uki-regret
•Matumizi ya sentensi fupi- Ni kibaya maze
Ni poa kuchill
•Kuchanganya msimo-Kuchill ;Ukiregret ;Ma-mission.
Tuza ½ kwa kila sifa inayotolewa na ½ alama kwa mfano (Jumla al.4)
(c)•Ukosefu wa msamiati.
•Kukubalika katika kikundi fulani.
•Kujitambulisha na lugha fulani au kuonyesha umahiri katika lugha zote mbili
(d)•Kutilia mkazo ufundishaji ufaao wa Kiswahili.
•Kupitishwa kwa sera nzuri inayoweka wazi malengo ya serikali kuhusu lugha hii.
•Kuhimiza kuwepo kwa idara za Kiswahili katika taasisi za juu ili kuendeleza utafiti.
•Raia kukumbushwa kuionea fahari lugha hii.
•Wachapishaji kuhimizwa kuchapisha machapisho ya Kiswahili.
•Vipindi vya redio na runinga viwepo vya kuhimiza matumizi fasaha ya Kiswahili.
•Kiswahili kuwa msingi muhimu katika taasisi za elimu. k.m.Daktari asiweze kuwa
daktari bila kuonyesha uwezo mzuri wa lugha ya Kiswahili.
8. (i) Sehemu za kuabudu/ ibada / mzungumzo ya Kristo
(ii)(a) Matumizi ya lugha iliyojaa upole/ unyenyekevu
(b) Msamiati maalum unaohusiana na dini Fulani. Kwa mfano ‚Yesu” okoka, ‚
Mungu asifiwe’ ‚ Halleluya, ‚ Amen’ dini ya kikikristo
(c) Huweza kuwapo matumizi ya maneo au makuu kutoka kwa Bibilia m.f. usiwe kama
Yona, Paulo na Sila. .
(d) Huwepo matumizi ya msamiati ambao unaeleweka tu katika muktadha huo wa
mazingira yanayohusika tu. Mungu anaendelea kunibariki. ‚Amen”
(e) Lugha haina matumizi ya misimu au hata lugha inayoonekana kama isiyozingatia
adabu; huwa lugha yenye tasfida.
(f) Majina yanayofungamana na ibada inayohusika, injili, sala, Mungu, Bwana asifiwe
(g) Matamshi au lafudhi ya utamkaji wa maneno kutegemea mazingira fulani ya ki-ibada
(i) Dini
(ii) Biashara
9. (a) Sajili ya bungeni
(b) Sifa
– Msamiati na istilahi huhusiana na bungeni k.m. vikao vya bunge, spika, mesi, karani n.k.
– Hurejelea sheria za nchi au katiba katika kutetea hoja fulani inayojadliwa
– Lugha ya heshima katika mawasiliano na majadiliano-Mheshimiwa spika
– Kuchanganya ndimi katika mijadala, ili kujieleza vyema
– Wabunge hutaja msamiati unaorejelea sheria na kanuni za bunge wanapojadiliana kuhusiana na maswala mbali mbali, hasa shughuli za kinidhamu (zozote 4 x 2= al. 8)
10.
kwa mfano Chakita, Chakike
Kilitangazwa kuwa mojawapo ya lugha za bunge
11 (a) – Kurejelea sura au aya za maandishi matakatifu kama Bibilia, kurani n.k.
– Kuna msamiati maalum kama kasisi, shehe, kadhi, hekalu, jehanamu n.k.
– Matumizi ya ishara za mwili hutamalaki. Haya hulenga kuwanasa wasikilizaji wa
kudunisha hali ya kusikiliza. s
– Matumizi ya lugha huhusisha kubadilikabadilika kwa sauti kutegemea madhumuni na
matakwa ya msemaji.
– Ni lugha ya upole na kunyenyekea.
– Kuwa na hali ya kuzungumza kwa pamoja hasa katika maombi
– Lugha inayotumiwa huwa ya wastani, isiyo ngumu kueleweka au nyepesi.
– Ni lugha ambayo mtu hapewi fursa ya kuuliza swali
– Ni lugha ya unyonge na hutumiwa sana wakati mtu/watu wamefikwa na msiba
(b) – Muktadha wa matumizi au mazungumzo
– Wahusika na uhusiano wao
– Umri wa wahusika
– vyeo vya wahusika wa mazungumzo
– Tabaka au nafasi ya kijamii ya wahusika wa mazungumzo
– Madhumuni ya mawasiliano au mazungumzo
– Mada zinazozungumziwa
– Jinsia ya wahusika wa mazungumzo
– Lugha aizungumzayo mzungumzaji
12. i) – Hii ni sajili ya magari ya uchukuzi
– Inatokea katika kituo cha matatu au barabarani gari linaposimama kubeba abiria
– Kuna utingo anayetangaza kiasi cah nauli kwa wasafiri wanaotaka kulipa malipo nafuu
ii) – Kuna matumizi ya lugha maalum kama 46, ingia twende shona
TAZAMA
13. a) Muktadha wa ndoa/ arusi/ kuzungumza juu ya mahari
b)
TAZAMA sarufi/ isimu jamii
Maswali na majibu ya isimu jamii pdf
isimu jamii questions
maswali ya isimu jamii atika school
maswali ya isimu jamii kcse
isimu jamii past papers
maswali ya sajili ya sokoni
isimu jamii full notes
maswali ya isimu jamii kidato cha pili